UTANGULIZI

Wanasayansi wa kijamii kutoka nchi za kaskazini ambao hufanya kazi katika bara la Afrika kwa muda mrefu wamekuwa wakitegemea maarifa na ustadi wa watafiti wa ndani na wasaidizi wa watafiti. Bila msaada huu, ingekuwa vigumu kwa wasomi wengi wa Kaskazini kusafiri hasa katika maeneo yasiyo salama na yenye vita. Walakini mienendo hii inakuwa kutoka kwa uhusiano wa nguvu za kikoloni, na hata leo watafiti kutoka nchi za Kusini wanajulikana sana kama warekebishaji tu, waogozaji, au wapokea data kwa wenzao wa Kaskazini, wakati wanapaswa kutambuliwa kama washiriki muhimu katika utafiti wa kitaaluma.

Mwanzoni mwa mwaka 2018 watafiti thelathini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Ulaya walikusanyika pamoja katika mji wa Bukavu huko mashariki mwa Kongo kujadili juu ya safu inayoendelea ya watafiti wa Kusini katika mizunguko ya kisiasa ya uzalishaji wa maarifa. Zaidi ya miaka miwili iliyofuata, kikundi hicho kiliungana tena mara kwa mara huko Bukavu kwa mfululizo wa semina kubwa. Katika mikusanyiko hii, washiriki walitafuta, walichunguza na kuanza kushughulikia masuala ya kimaadili yanayotokea wakati watafiti wa Kaskazini wanashirikiana na wenzao kutoka Kusini kufanya kazi katika maeneo yenye vita au maeneo yaliyokuwa na vita.

Tafakari hizi zilisababisha kuundwa kwa “Mijadala ya Bukavu” mradi wa blogi unaosimamiwa na Mtandao wa Utawala katika Migogoro (GIC) ambao unakusudia kuwapa nafasi wale ambao mara nyingi hubaki wametengwa au wasioonekana katika utoaji wa taarifa. Mnamo mwaka 2020, blogi hizi zilikusanywa katika kitabu kiitwacho “Mijadala ya Bukavu”, kuelekea kuondoa ukoloni wa utafiti wa kitaaluma. Mchoraji mashuhuri wa kisiasa wa Kongo aitwae Tembo Kash alijiunga na mradi huo akiunda katuni zinazoonyesha mada kuu za kitabu hicho. Vielelezo vyake katika kitabu cha “Mijadala ya Bukavu” ndio msingi wa maonyesho haya ya kidijitali.

Katika mikusanyiko hii, washiriki walitafuta, walichunguza na kuanza kushughulikia masuala ya kimaadili yanayotokea wakati watafiti wa Kaskazini wanashirikiana na wenzao kutoka Kusini kufanya kazi katika maeneo yenye vita au maeneo yaliyokuwa na vita.

Insha katika kitabu cha “Mijadala ya Bukavu” zinachunguza udhaifu wa mtafiti wa ndani na zinajadili kuhusu suala la uandishi katika ushirikiano wa Kaskazini na Kusini, zinahitaji uwajibikaji mkubwa kwa jamii na kuleta mjadala kuhusina na mambo ambayo yamekuwa yakipuuziwa wakati wa kazi ya utafiti wa kielimu ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo.

Mawazo yaliyowasilishwa katika insha hizi na yaliyoonyeshwa wazi na sanaa za Kash hutumika kama mashtaka ya vurugu za kimuundo ambazo zinaendelea katika mchakato wa uzalishaji wa maarifa ya kitaaluma. Wanasema kuwa mchakato huu ni kati ya mambo ambayo yanahusu kuondoa utu na ufutaji wa watafiti kutoka Kusini. Wakati huo huo, hutoa maoni ya kufundisha juu ya jinsi watafiti kutoka Kusini wanaweza kuhusishwa katika mchakato wa utafiti kama washirika kamili na sauti zao mwishowe kusikika. Kama watafiti wenyewe wanavyotuambia, kwa kutumia ujuzi wetu kutimiza majukumu yetu katika kazi za utafiti kwa kushirikiana tunaweza kuleta maendeleo kwa kuondoa ukoloni wa utafiti na kujenga ushirikiano bora.

Mawazo yaliyowasilishwa katika insha hizi na yaliyoonyeshwa wazi na sanaa za Kash hutumika kama mashtaka ya vurugu za kimuundo ambazo zinaendelea katika mchakato wa uzalishaji wa maarifa ya kitaaluma.

Mradi huu ni ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Ghent na Chuo kikuu cha kikatoliki cha Louvain huko Ubelgiji, na Taasisi ya Angaza yenye makao yake mjini Bukavu na Kikundi cha Mafunzo na Usalama wa Binadamu. Ilifadhiliwa na ARES na pia ilipata msaada kutoka kwa Mpango wa Utafiti wa Migogoro na Kituo cha Mamlaka ya Umma na Maendeleo ya Kimataifa katika shule ya Uchumi na Sayansi ya Siasa ya London.

Copyright © 2022 by bukavuseries.com and Tembo Kash. All rights reserved. This website, images, content or any portion thereof may not be reproduced or used in any manner whatsoever without the express written permission of the publisher. For more information contact: intdev.crp@lse.ac.uk

Terms of Use