TEMBO KASH
Mzaliwa wa Butembo, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Tembo Kash alimaliza masomo yake ya msingi na sekondari katika mji wa Beni. Baada ya kupata diploma yake ya Falsafa ya Kilatini, alienda Kinshasa ambapo alijiandikisha katika Chuo cha Sanaa mnamo mwaka 1987. Miaka mitatu baadaye alitunukiwa shahada ya Sanaa ya Picha ya matangazo (sasa ni mawasiliano ya kuonekana)
Pamoja na ubunifu wake wa vichekesho, Kash anaweza kudai kuwa ndiye mchoraji katuni wa kwanza kujihusisha na siasa za Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo, kuanzia mwaka 1990 alifanya kazi katika gazeti lijulikanalo kwa jina la ‘ Le phare’. Kuanzia mwaka 1991 hadi mwaka 2005 akishirikiana na marafiki wengine wa kitamaduni, alisaidia kuandaa matoleo matano ya Maonyesho ya Kiafrika ya Usomaji na Vitabu kwa Vijana.
Kuanzia mwaka 1992 hadi leo Kash ametumia studio yake kufanya kazi kama mchoraji wa matangazo kwa watangazaji mbalimbali. Katika miaka 20 iliyopita amefanya kazi yake huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kongo Brazzaville, Ufaransa, Ubelgiji, Luxemburg, Moroko, Niger, Vietnam, Reunion, Mauritius, Algeria, Kameruni na Guinea-Conakry
Copyright © 2022 by bukavuseries.com and Tembo Kash. All rights reserved. This website, images, content or any portion thereof may not be reproduced or used in any manner whatsoever without the express written permission of the publisher. For more information contact: intdev.crp@lse.ac.uk