MIJADALA YA BUKAVU

Watafiti waliotoweshwa

Ingawa ujuzi wao ni muhimu katika shughuli nzima ya utafiti, watafiti wasaidizi katika nchi za kusini mara nyingi huchukuliwa kama wakusanyaji wa data tu, na majina yao hufutwa wakati wakuchapa miradi hiyo hiyo ambayo walifanya. Kwenye picha hapo juu, Tembo anaonyesha jaribio hili la kufutwa kwa kutuonyesha mtafiti wa Kongo ambaye, anajitazama kwenye kioo cha kitaaluma na kugundua kuwa ametoweka kabisa na kilichosalia ni mkoba wake wa utafiti tu. Taaluma inaonekana kuhitaji data alizokusanya lakini haimthamini yeye kama mtafiti. Waandishi wengi katika safu ya Bukavu wanapambana na suala hili katika maandishi yao labda hakuna zaidi ya Elisée Cirhuza katika insha yake. “Taken out of the picture? The researcher from the Global South and the fight against ‘academic neo-colonialism’” na Aymar Nyenyezi Bisoka katika “Can silent voices speak? When power relationships govern the conditions of speech.”

NIRUDISHE KATUNINI

Habari sio bure

Kuwalipa watafiti wasaidizi ili kupata taarifa inabezwa kwa ujumla na inaonekana kuweka ukweli na ubora wa data hiyo katika hatari. Kwa sababu hiyo, wasimamizi wa miradi wa nchi za Kaskazini hukwepa kuweka malipo hayo katika bajeti ya miradi yao. Vilevile watafiti wa Kongo wamekuwa wakipata wakati mgumu na Viongozi wa serikali za mitaa na hata wanajamii ambao wanaamini kwamba utoaji taarifa ni njia ya kupata kipato. “When you become Pombe Yangu (My Beer): Dealing with the financial expectations of research participants,” Jérémie Mapatano anafafanua ugumu unaojitokeza katika kukabiliana na wahojiwa wanodai malipo. Wakati huo huo, katika insha ya pamoja, “In the presence of white skin: the challenges arising from people’s expectations when encountering white researchers in the field,” Élisée Cirhuza Balolage na Esther Kadetwa Kayanga wamechunguza ni namna gani uwepo wa watafiti wakigeni unaweza kuongeza matarajio ya fedha kwa washiriki.

NIRUDISHE KATUNINI

Matukio ya kutisha wakati wa utafiti

Insha nyingi za Bukavu zinahusika na shida za kisaikolojia katika maeneo ya mizozo na kuwa inaweza kuchukua muda kufanya utafiti. Kwa wakati “When the backpack is full: the omertà surrounding the psychological burdens of academic research,” An Ansoms anaandika kwamba shida hizi zinazidishwa zaidi na utamaduni wa ukimya katika akademia. Kuna nafasi chache ambazo watafiti wanaweza kuonyesha mazingira magumu na kuzungumza waziwazi juu ya changamoto wanazoshuhudia au kupata wakati wa kazi zao. Badala yake, watu wanatarajiwa kubeba mizigo yao ya kisaikolojia kimya na kuonyesha uso wa kijasiri kwa wenzao. Katika picha hii ya kejeli, Kash anaonyesha mtafiti wa Kongo na mgeni wakihimizwa kuamini kwamba mifupa ya binadamu waliyokutana nayo ni mifupa ya bonobo tu, badala ya athari dhahiri za vita ya hivi karibuni. Ansams anamalizia insha yake kwa kutoa wito na kupendekeza kubadili utamaduni wa ukimya kwenda katika ule wa uwazi na kuungana mikono katika kazi.

NIRUDISHE KATUNINI

Unyanyasaji wa watafiti wa kike

Katika insha yake “The challenges facing female researchers in conflict settings,” Irène Bahati anachunguza changamoto mahususi za watafiti wanawake wanazokabiliana nazo katika maeneo yao ya kazi huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Katika picha hii, Kash amechagua kuonyesha juu ya masuala ambayo Bahati ameyasema kwamba, watafiti wa Kongo wanakabiliwa na watu (na wakati mwingine hata wanawake wengine) ambao wanatarajia watangulize majukumu ya nyumbani badala ya matakwa ya kitaaluma.

NIRUDISHE KATUNINI

Kuthamini data kuliko maisha

Katika safu yote ya Bukavu, waandishi wanaangazia ukweli kwamba watafiti wa ndani na wasaidizi wa utafiti nchini Kongo mara nyingi huthaminiwa tu kwa data wanazokusanya. Mara chache hupewa nafasi ya kushiriki kama washirika kamili katika miradi ya utafiti wanayofanya. Mbaya zaidi hata usalama wao haupewi kipaumbele, bali hutakiwa kukusanya data ambazo washirika wao wa Kaskazini wanahitaji. Hili ni moja ya maswala ambayo Alice Mugoli Nalunva anagusia katika insha yake, “Between Passion and Precarity: the work of a researcher in the DRC.” Katika katuni iliyoonyeshwa hapa, Tembo Kash anaonyesha mada hii ya picha ya mtafiti wa Kongo ambaye amefanikiwa kutoka kwenye mashua iliyopinduka. Wakati mtafiti anapiga simu kuripoti kile kilichotokea, anagundua kuwa bosi wake anajali tu usalama wa data za mradi.

NIRUDISHE KATUNINI

Kutokuwepo kwa mkakati dhidi ya kutekwa nyara

Wasimamizi wa miradi iliyoko Kaskazini mara nyingi hushindwa kutambua kuwa kazi katika maeneo yenye vita inaweza kuweka watafiti kwenye hatari kubwa. Kutozingatia usalama wa watafiti wa Kongo ni suala linalojirudia kwa wingi katika ya Bukavu. Katika insha yao ya pamoja Work Without Pay? A critical look at the contracts and lived experiences of local researchers in the DRC, Élisée Cirhuza, Irène Bahati, Thamani Précieux Mwaka na An Ansoms wanasema, kwa mfano, mikataba ya utafiti sio tu inashindwa kutoa malipo kwa watafiti wa Kongo, lakini pia hupuuza usalama wa watafiti wa ndani wakati wa kazi zao kwenye maeneo ya kazi. Wakati huo huo, “Surviving Intimidation: When having your research challenged upends your life as researcher”, Bosco Muchukiwa anaonyesha hata wakati wa kufanya kazi kwenye miradi yao wenyewe, watafiti katika nchi za Kusini wanakabiliwa na hatari ambazo wenzao wa Kaskazini hawakumbani nazo. Katika katuni hii, Kash anaonyesha ukosoaji wa Cirhuza et al. kwa kuonyesha msimamzi wa kigeni wa mradi ambaye anamwambia msaidizi wake wa utafiti aliyetekwa nyara kuwa hakuna bajeti iliyopo ya kulipa fidia yake na kumwokoa, lakini mipango inaweza kufanywa kurudisha data alizokusanya.

NIRUDISHE KATUNINI

Ukosefu wa usawa katika uandishi wa kitaalamu

Suala la kufutwa kiakademia ni moja wapo ya mada endelevu za safu ya Bukavu. Mara kwa mara wachangiaji wa safu wanaelezena namna wamekuwa wakitolewa kwenye nafasi ya kukusanya data licha ya utaalamu mwingi walionao na njia muhimu wanazozijua katika mchakato wa utafiti. Katika katuni hii, Kash anaangazia jambo hili kwa kuonyesha mtafiti mchanga akimwonyesha bosi wake utafiti na uchambuzi mwingi alioufanya, na kuambiwa kuwa kazi yake ni kukusanya data na kuzikabidhi na si vinginevyo. Katika “‘They stole his brain’: The local researcher – a data collector, or researcher in his own right?”, Stanislas Bisimwa Baganda anahoji ni kwanini watafiti wa eneo hilo hawahusishwi kwenye machapisho wakati miradi mingi ya utafiti haiwezekani bila maoni yao kama wawezeshaji na wachangiaji.

Vivyo hivyo, katika insha yake “‘Donor-Researchers’ and ‘Recipient-Researchers’: bridging the gap between researchers from the Global North and Global South”, Judith Buhendwa Nshobole anasema kuwa watafiti wa Kaskazini wana jukumu la kufanya utoaji wa elimu uwe wa usawa kwa kujumuisha watafiti wa kusini kwenye hatua zote za miradi ya utafiti. Wakati huo, katika “‘These Phantom Researchers’: What of their visibility in academic publications?”, Bienvenu Mukungilwa anaonyesha kwamba ukiondoa watafiti wadogo kwenye mchakato wa uchapishaji husababisha upotevu wa fursa kwa watafiti na timu nzima ya utafiti. Mwisho, katika “We Barely Know These Researchers from the South! Reflections on Problematic Assumptions about Local Research Collaborators”, Emery Mudinga anahoji watafiti wa ngazi za juu kubadili mtazamo wao juu wa watafiti wao wasaidizi na wachangiaji, kwa kusema kuwa hii ni hatua ya kwanza kuelekea kushughulikia na kurekebisha suala la kufutwa kwa watafiti wasaidizi kitaaluma.

NIRUDISHE KATUNINI

Kuwekewa ajenda za kiulaya

Katika picha hii, Kash anaangazia suala la wasimamizi wa miradi kutoka nchi za Kaskazini kupuuza utaalamu wa watafiti wa eneo hilo, na badala yake wanaamuru jinsi watafiti wa ndani wanapaswa kufanya utafiti wao. Hapa mfanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali anampa mtafiti wa Kongo “Ujumbe maalumu” ambao unamwelekeza jinsi anapaswa kufanya mradi huo na ni hitimisho gani anapaswa kufikia kabla hata hajaanza utafiti wake. Katika insha yake, “‘A research assistant is just an implementer’: the argument in favor of involving local researchers in project design”, Vedaste Cituli Alinirhu inatafakari juu ya kile kinachopotea wakati watafiti wa ndani wameondolewa kwenye mchakato wa kubuni miradi ya utafiti na badala yake wanatarajiwa kutekeleza tu maoni ya wengine. Akiandika katika “The NGO-ization of Academic Research”, Pierre Basimise Ngalishi Kanyegere anatoa hoja kwamba kulazimisha malengo ya utafiti kutoka juu kwenda chini ni kupuuza utaalamu wa ndani, wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali hufanya vibaya sio tu kwa watafiti wa ndani, bali pia kwa malengo yao ya utafiti. Katika “Escaping Big Brother’s gaze in research in the Global South”, Joël Baraka Akilimali anaonyesha kuwa mienendo kama hiyo hufanyika kwenye duru za kitaaluma. Mwisho, kwenye maandiko ya makubaliano kutoka kwa mtazamo wa Kaskazini, katika “Can collaborative research projects reverse external narratives of violence and conflict?”, Koen Vlassenroot anasema kuwa muundo uliopo wa ushirikiano wa utafiti wa Kaskazini na Kusini unahitaji kupitiwa ili kuwapa watafiti wa ndani sauti kubwa katika utafiti na uchambuzi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

NIRUDISHE KATUNINI

Hatari, vitisho, na maadili ya kudhaniwa ni mpelelezi

Ukusanyaji wa data katika maeneo ya vita au maeneo yenye usalama mdogo ni kazi inayohitaji umakini, uwezeshaji na uelewa mzuri wa muktadha wa eneo. Katika “Navigating Armed Conflict Zones”, Josaphat Musamba anatoa utangulizi kwa wasomaji juu ya changamoto zinazohusika na kufanya utafiti katika eneo la vita, na anaelezea mikakati mingine ya ubunifu ambayo watafiti wa ndani hutumia kukabili vizuizi katika maeneo ya kazi. “He’s hiding under his hat! Going in disguise to collect data in the field,” Précieux Thamani Mwaka, Stanislas Bisimwa Baganda na An Ansoms wanaelezea baadhi ya changamoto ambazo watafiti wa Kongo wanakutana nazo wakati wa kufanya kazi na wahojiwa ambao wana mashaka na utafiti wao. Wanaendelea kujadili suluhisho ambazo watafiti hupata juu ya changamoto hizi na pia hatari wanazopata, na maeneo ya kimaadili wakati mwingine wanachagua kuficha ukweli kwamba wao ni watafiti. Wakati huo huo, katika “When an Armed Guide is Imposed on You: Navigating Research in a Conflict Zone,” Eric Batumike Banyanga anaonyesha kile kinachoweza kutokea kwa mtafiti wakati tuhuma zinafika hatua mbaya, akisimulia uzoefu wake mwenyewe wa kufanya kazi chini ya ulinzi mkali wa walinzi wenye silaha. Katika picha iliyoambatanishwa, Tembo Kash anaonyesha jinsi mivutano inaweza kuongezeka haraka kati ya watafiti na wahojiwa ikiwa tuhuma zinatokea kati ya pande hizo mbili.

NIRUDISHE KATUNINI

Kufanya kazi bila muda wa kutosha

Wakati watafiti wa ndani na wasaidizi wautafiti wakiendelea kufanya kazi za kitafiti nchini Kongo, watafiti wa Kaskazini wanaendelea kuamuru kuhusu muundo, ratiba na malengo ya miradi mingi ya utafiti nchini. Hivyo basi waandaaji miradi huwa mbali na ukweli wa mambo yanavyoenda kwenye maeneo husika na wengi huweka madai na matarajion yasiyo ya kweli kwa wenzao wa Kusini. Wakati huo huo watafiti wa Kusini mara nyingi huhisi hawawezi kupinga mahitaji haya kwa sababu ya kukosekana kwa usawa katika nguvu, rasilimali, ufadhili n.k. Kama Kash anavyoonyesha katika mfano huu shinikizo kama hizo wakatimwingine zinaweza kuwalazimisha watafiti wa eneo hilo kufanya maamuzi ya kutiliwa shaka kimaadili katika kazi zao. Kwa uchunguzi dhahiri na wa busara wa mienendo hii angalia insha ya Esther Kadetwa, “Reliable data? The pressure to deliver, versus the complexities of the field,” na ya Élisée Cirhuz, “Remunerating researchers from the Global South: a source of academic prostitution?”

NIRUDISHE KATUNINI

Kutambua tofauti za kitamaduni

Kufanya mazoezi ya kazi na timu yenye tamaduni nyingi hutengeneza fursa nyingi za kujifunza na kubadilishana uzoefu. Wakati huo huo, ushirikiano kama huo unaweza kusababisha kutofautiana kwa kitamaduni na kusababisha mivutano ndani ya timu. Katika insha yake, “Lost in translation? Managing cultural differences in the face of risk in the field”, Dieudonné Bahati Shamamba anasimulia uzoefu wake akifanya kazi katika vikundi vya watafiti wa Wakongo na wageni, na anaangazia njia za washirika kujenga namna bora za uelewa kweye mgawanyiko wa kitamaduni. Hapa, Tembo Kash anaonyesha kutokubaliana na umuhimu wa dini ndani yatimu ya watafiti wa tamaduni nyingi baada ya tukio la kutisha. Picha hii kifupi inawakilisha insha ya Shamamba.

NIRUDISHE KATUNINI

Kutafiti ‘nyumbani’ bila kuweka maoni yako

Waandishi kadhaa katika safu ya Bukavu hutafakari juu ya kiwewe, hofu, na hatia wanayoipata wakati wa kazi katika maeneo ya kazi. Tofauti na watafti kutoka nchi za kaskazini, watafiti wa ndani na wasidizi wa utafiti huko Kongo mara nyingi wanaungana na jamii ambazo wanaulizwa na jamii ambazo wanatakiwa kufanya utafiti. Wakati watafiti wa kigeni wanaweza kudumisha kiwango cha kujitenga kutoka kwa hali wanazosoma katika maeneo ya kazi, mara nyingi watafiti wa ndani huko hawana fursa hii. Katika insha yake “The egocentricity of field ethics: questioning otherness, decency and responsibility,” Anuarite Bashizi anapambana na hatia na dhiki yeye na watafiti wengine wa Kongo wanapata wanapokabiliana na mateso ya watoa habari wao wakati wa kazi. Vivyo hivyo, “Epistemological rupture, detachment, and decentering: requirements when doing research ‘at home’” Francine Mudunga anachunguza changamoto za maadili za watafiti wa eneo wanakabiliwa nazo wakati kazi yao inahitaji kuwachukulia kwa umbali hisia kutoka kwa wahojiwa katika jamii ambazo wao wenyewe wanaweza kuwa na uhusiano. Wakati huo huo, “Waiting for the morning birds: researcher trauma in insecure environments”, Thamani Mwaka Précieux anasimulia jinsi, ambavyo washiriki wa jamii zilizoathiriwa na mizozo, wasaidizi wa utafiti wa ndani wakati mwingine hata Maisha yao yanawekwa hatarini wakati wa kufanya utafiti.

NIRUDISHE KATUNINI

Shinikizo la kisaikolojia

Katika insha yake “Research, or Adventure? The lived experiences of researcher assistants”, François-Merlan Zaluke Banywesize anaangazia juu ya matakwa yasiyo halisi ya wafadhili na wasimamizi kutoka nchi za Kaskazini, hupelekea watafiti wa ndani kujihisi kulemewa na kuzidiwa na shughuli za utafiti.  Hapa, Tembo Kash anaonyesha kwa kushangaa suala hili kwa kuonyesha majadiliano kati ya mtafiti wa Kongo ambaye anahisi kushinikizwa kuchukua mradi mpya, na mkewe anafadhaika sana na usumbufu, hali ya kimwili na taabu ya mume wake katika kazi hizo.

NIRUDISHE KATUNINI

Kufanya kazi katika maeneo yanayotawaliwa na wanaume

Ingawa wote walikuwa tayari wameandika machapisho kwenye blogi ya Bukavu, wakati mradi unaendelea, An Ansoms na Irène Bahati wanagundua kwamba mada muhimu imebaki ambayo haijafanyiwa uchunguzi katika safu hii kwenye mwendelezo wa utafiti juu ya changamoto za usalama na mahisi watafiti wanazokabiliana nazo maeneo ya kazi. Wakidhani kwamba uzoefu maalumu wanaopitia watafiti wanawake unahitaji umakini zaidi, wanawake hao wawili walishirikiana kuandika insha kuhusu suala hili. Katika “When the room is laughing: from female researcher to researcher-prostitute,” Ansoms na Bahati wanashuhudia unyanyasaji na vitisho ambavyo wanawake wanakabiliana navyo maeneo ya kazi kama matokeo ya jinsia zao, na kueleza mikakati ambayo watafiti wa kike wanapaswa kutumia ili kuepuka mambo hayo, na wanatoa wito kwa ulimwengu wa kitaaluma kutambua na kuanza kushughulikia udhaifu fulani wa watafiti wakike katika maeneo hayo ya kazi. Katika picha hii, Tembo Kash anatumia baadhi ya mawazo ya Ansoms na Bahati katika picha moja inayoonyesha viwango vya utafiti ambavyo hubadili muelekeo pale ambapo askari wawili wanapoleta utani wa kimapenzi katika kuoa majibu yao kwa watafiti wanawake.

NIRUDISHE KATUNINI

Kutafuta ushirikiano wenye usawa

Machapisho ya Bukavu yamekuwa kama sehemu ya uchunguzi juu ya changamoto za kimaadili zinazotokea wakati watafiti wa Kusini na Kaskazini wakifanya kazi kwa pamoja. Katika insha yake “‘Businessisation of Research’ and Dominocentric Logics: Competition for Opportunities in Collaborative Research,” Godefroid Muzalia anaeleza uzoefu wake wa miaka nane ya kazi kwa ushirikiano na watafiti wa Kaskazini na Kusini, akiwa kama msimamizi wa Kusini wa miradi ambayo masharti na ufadhili wake umeamriwa kutoka Kaskazini. Wakati huo huo, “Umoja ni nguvu: towards more equitable collaborative research,” Josaphat Musamba na Christoph Vogel wanatafakari pamoja juu ya uzoefu wao wa kujenga ushirikiano sawa (na urafiki) katika kipindi cha takribani miaka kumi ya utafiti wa pamoja nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Katika maelezo yake yaliyoko kwenye blogi hizi mbili, Tembo Kash anaonyesha ushirikiano wa watafiti wa Kaskazini na Kusini kwa misingi wa kushirikiana na kuheshimiana. Walakini anatuonyesha kuwa ushirikiano kama huo ni sehemu moja tu ya suluhisho la kuendelea kwa mawazo ya kikoloni katika uzalishaji wa maarifa. Ili ukoloni kamili utokomee, lazima pia tukabiliane na miundo mibaya ya kielimu ambayo dhana zenye ubaguzi juu ya watafiti katoka nchi za Kusini huendelea kuwa kawaida.

NIRUDISHE KATUNINI

Kupishana kwa watafiti na wahojiwa

Insha kadhaa katika safu ya Bukavu zinaangazia hali ya upekuzi wa utafiti katika hali zisizo salama, ikikosoa tabia ya timu za utafiti kukusanya data kutoka kwa jamii bila kufuata tena kuwajulisha wahojiwa matokeo ya tafiti zao. Wakati watafiti kutoka nchi za kaskazini kwa kawaida hurudi katika nchi zao baada ya mradi, wasaidizi wao na washirika wao hubaki wakiwasiliana na wanaweza kuendelea kufanya kazi nyingine na wahojiwa wa zamani. Kwa hivyo, watafiti wa eneo lazima wakabiliane na changamoto na uchovu wa utafiti kwa washiriki wao kwa njia ambayo watafiti kutoka nchi za Kaskazini hawalazimiki kufanya. Katika insha zao “‘Hold on; we’re still thinking it through.’ When will we get a report on your findings?” na “’Give Me Back My Words’: reflections on a forgotten aspect of participant follow-up” Christian Chiza Kashurha na Isaac Bubala Wilondja kila mmoja anaelezea kufadhaika kwake kwa kutoweza kutoa jamii zinazoshiriki matokeo kutoka kwa miradi wanayoshiriki. Waandishi wote waili wanasema kuwa watafiti wa Kongo mara nyingi hukosa nguvu ya kuwawajibisha wasimamizi wa miradi kutoka nchi za Kaskazini kuwajibika kwa jamii ambazo utafiti unafanywa. Kwa hivyo kila mmoja huwaita watafiti wa Kaskazini kwao wenyewe kutafakari kwa kina Zaidi juu ya mchakato wa uzalishaji wa maarifa, na kuzingatia ni nani maarifa hayo yamekusudiwa.

Wakati huo huo, katika insha yake, “‘Come back later.’ – ‘On what day?’ – ‘Just, come back!’”, Irène Bahati anaandika uchungu ambao wahojiwa katika jamii zilizotafitiwa kupita kiasi wanahisi kuulizwa mara kwa mara kushiriki katika masomo ambayo majibu yao hayaonekani kamwe. Vivyo hivyo, katika “The ‘Researcher-Glutton’: Data collection in insecure settings in the Global South”, Espoir Bisimwa Bulangalire anaonyesha jinsi hasira katika jamii zinazojibu zinaweza kukua kuwa chuki na hata uhasama kwa watafiti wa ndani, ambao mara nyingi huonekana zaidi wakifanya miradi ya utafiti, licha ya kuwa na athari kidogo katika tafiti wanazofanyia kazi. Hapa, Tembo Kash anatumia picha ya mazungumzo magumu kati ya msaidizi wa utafiti wa Kongo na mtu anayetakiwa kujibu kuonyesha mada zinazohusiana zinazochunguzwa na insha hizi nne.

NIRUDISHE KATUNINI

Copyright © 2022 by bukavuseries.com and Tembo Kash. All rights reserved. This website, images, content or any portion thereof may not be reproduced or used in any manner whatsoever without the express written permission of the publisher. For more information contact: intdev.crp@lse.ac.uk

Terms of Use