Bukavuseries

  • NYUMBANI
  • UTANGULIZI
  • MAONYESHO
  • MAELEZO
  • BLOGI
  • KITABU
  • WATAFITI
  • TEMBO KASH
  • English
  • Français

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

test via plugin

READ MORE

 

“Mtafiti kutoka nchi za Kusini kwa kiasi kikubwa bado haonekani katika matokeo ya utafiti, na pia katika machapisho ya utafiti.”

Élisée Cirhuza, “Taken out of the picture? The researcher from the Global South and the fight against ‘academic neo-colonialism’”

NIONYESHE ZAIDI

“Wasomi wachache wanafahamu ukweli kwamba ukoloni wa maarifa unawahusisha wao binafsi.”

Aymar Nyenyezi Bisoka, “Can silent voices speak? When power relationships govern the conditions of speech.”

NIONYESHE ZAIDI

“Bwana, acha kuja hapa kutajirika kupitia migongo ya wengine. Utafiti wako utakapomalizima utapata diploma yako na upewe heshima na upate kutambuliwa na sifa nzuri wakati mimi naendelea kubaki nyuma sina furaha hapa kijijini.”

Jérémie Mapatano, “When you become Pombe Yangu (My Beer): Dealing with the financial expectations of research participants”

NIONYESHE ZAIDI

“Wafiti hawachukuliwi kama watafiti tu bali pia wafadhili wawakilishi na hivyo huongeza matarajio kwa wahojiwa. Moja ya madhara ni kutokubali kuhujiwa au kutoa maelezo bila malipo ya kifedha.”

Élisée Cirhuza Balolage & Esther Kadetwa Kayanga, “In the presence of white skin: the challenges arising from people’s expectations when encountering white researchers in the field”

NIONYESHE ZAIDI

“Wengi wamepata matatizo ya afya ya akili kutokana na ukatili waliofanyiwa au kushuhudia au kwa kuhisi kukosa msaada kutokana na dhuluma walizofanyiwa.”

An Ansoms, “When the backpack is full: the omertà surrounding the psychological burdens of academic research”

NIONYESHE ZAIDI

“Ni mwenendo katika duru zetu kudharau watafiti wanawake kwa hoja zilizovumbuliwa kuwa na mizizi. Hii hufanyika zaidi kati ya wapendwa wetu katika ngazi ya familia na marafiki na kati ya wenzetu, ambao hutoa maoni kama, ‘Atafanyaje kazi za nyumbani wakati anafanya kazi ya aina hii?’ Wakati mtafiti mwanaume anaonekana kama mwezeshaji.”

Irène Bahati, “The challenges facing female researchers in conflict settings”

NIONYESHE ZAIDI

“Watafiti wa ndani hufanya kazi maeneo yao ya kazi, lakini hatari wanazokabiliana nazo mara nyingi hupuuzwa. Katika tukio la ugonjwa, utekaji nyara, au ajali makamishna wa utafiti kawaida hukataa majukumu hayo.”

Alice Mugoli Nalunva, “Between Passion and Precarity: the work of a researcher in the DRC”

NIONYESHE ZAIDI

“Mshirika (asiye msomi) anayeishi Kanada na pia ni mtu wa jamii yangu, alikuwa wa kwanza kunipinga. Alisambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akihoji tafiti zangu. Lakini zaidi ya kupinga tu utafiti wangu alituma kundi la watu wenye silaha kuniua.”

Bosco Muchukiwa, “Surviving Intimidation: When having your research challenged upends your life as researcher”

NIONYESHE ZAIDI

“Mikataba ya utafiti mara chache hujumuisha kifungu cha usalama wa watafiti zaidi juu ya afya akili. Wajibu wa mambo haya hubaki kwa watafiti binafsi.”

Élisée Cirhuza, Irène Bahati, Thamani Précieux Mwaka & An Ansoms,“Work Without Pay? A critical look at the contracts and lived experiences of local researchers in the DRC”

NIONYESHE ZAIDI

“Ni wazi kuwa bado hakuna usawa mkubwa wa mgawanyo wa madaraka na kanuni zisizo na tija ndani ya duru ya taaluma. Kwasababu ya dhana zisizo na msingi, kazi ya wasaidizi wa utafiti maranyingi haionekani.”

Emery Mudinga, “We barely know these Southern researchers! Reflections on some harmful assumptions about Southern research collaborators”

NIONYESHE ZAIDI

“Hali hii inaleta aina ya ukoloni wa kitaaluma ambao unashindwa kumtambua msaidizi wa utafiti kama mshirika ambaye haki zake ni sawa na za wenzao kutika nchi za Kaskazini.”

Stanislas Bisimwa Baganda, “‘They stole his brain’: The local researcher – a data collector, or researcher in his own right?”

NIONYESHE ZAIDI

“Je! Hawapaswi kuwa na fursa ya kuwa sehemu ya hatua za utafiti hata baada ya kuwasilisha ripoti? Mtazamo huu huenda ukafungua milango na kuwaruhusu kufanya maendeleo ya kitaalamu.”

Judith Buhendwa Nshobole, “‘Donor-Researchers’ and ‘Recipient-Researchers’: bridging the gap between researchers from the Global North and Global South”

NIONYESHE ZAIDI

“Kwa kupuuza muhusika muhimu ambaye anajua data vizuri kuliko mtu yeyote mtu huishia kukosa maoni muhimu na mitazamo ya uchambuzi.”

Bienvenu Mukungilwa, “‘These Phantom Researchers’: What of their visibility in academic publications?”

NIONYESHE ZAIDI

“Mara nyingi viongozi wa mradi hutumia wasaidizi wa utafiti kama wakusanyaji wa data tu, bila kwanza kuwashirikisha katika tafakari za kiutaratibu au kuwapa nafasi ya kutoa mwelekeo mzuri kwa wenzao wa kigeni.”

Vedaste Cituli Alinirhu, “‘A research assistant is just an implementer’: the argument in favor of involving local researchers in project design”

NIONYESHE ZAIDI

“Maswala ambayo Mashirika yasiyo ya Kiserikali hulenga hayana uhusiano wowote na hali halisi au shida halisi ambazo watu hupata, bali hutolewa na vipaumbele vya shirika.”

Pierre Basimise Ngalishi Kanyegere, “The NGO-ization of Academic Research”

NIONYESHE ZAIDI

“Udharau wa fikira za Kiafrika kwa dhana za Magharibi umekua ukitoka kuanzia kwenye miradi ya ufundishaji kupitia miradi ya utafiti hadi kufikia hatua ya kuchapishwa kwa majarida ya Magharibi yanayodhaniwa kuwa mazuri.”

Joël Baraka Akilimali, “Escaping Big Brother’s gaze in research in the Global South”

NIONYESHE ZAIDI

“Ushirikiano wa kweli sio tu wa kufanya mambo pamoja katika kila hatua, kuunda mradi na kuandika mapendekezo, inamaanisha kuuliza mifumo ya rejea na njia za utekelezaji.”

Koen Vlassenroot, “Can collaborative research projects reverse external narratives of violence and conflict?”

NIONYESHE ZAIDI

“Ikiwa watendaji katika maeneo ya kazi wanamwona mtafiti kama mpelelezi au kumwona kama tishio kwa sababu ya mikutano au mahojiano basi kuna sababu ya kuogopa kwamba mradi mzima wa utafiti utawekewa mashaka. Hatimaye inaweza pia kuweka maisha ya mtafiti katika hatari.”

Josaphat Musamba, “Navigating Armed Conflict Zones”

NIONYESHE ZAIDI

“Ikiwa kujificha kumebainika, watafiti wanapaswa kujielezeaje? Je! Kuna maana gani ya kukusanya data kwa kujificha kweye mtazamo wa maadili?”

Précieux Thamani Mwaka, Stanislas Bisimwa Baganda and An Ansoms, “He’s hiding under his hat! Going in disguise to collect data in the field”

NIONYESHE ZAIDI

“Kitendo rahisi cha kuwapo au kuuliza maswali kwenye mada fulani kinaweza kusababisha mzozo mpya na/au kufufua iliyopo.”

Eric Batumike Banyanga, “When an Armed Guide is Imposed on You: Navigating Research in a Conflict Zone”

NIONYESHE ZAIDI

“Ushiriki wa msaidizi wa utafiti hauishii kwenye ukusanyaji wa data peke yake, msaidizi lazima mara nyingi afanye kazi chini ya shinikizola ratiba iliyowekwa na wafadhili ambao wanaweza kosa uelewa wa kutosha wa hali halisi.”

Esther Kadetwa, “Reliable data? The pressure to deliver, versus the complexities of the field”

NIONYESHE ZAIDI

“Taasisi za masomo na utafiti lazima ziongoze katika kuboresha malipo ya watafiti kutoka nchi za Kusini kwa kuzingatia ugumu na hatari zinazojitokeza maeneo ya kazi.”

Élisée Cirhuza,“Remunerating researchers from the Global South: a source of academic prostitution”?

NIONYESHE ZAIDI

“Kwake kilio chotechote cha msaada wa kimungu wakati wa hofu kilikuwa hakimaanishi chochote. Wakati magumu mawasiliano ya kweli ya tamaduni nyingi yamekuwa changamoto kubwa.”

Dieudonné Bahati Shamamba, “Lost in translation? Managing cultural differences in the face of risk in the field”

NIONYESHE ZAIDI

“Kwa hiyo kuna mvutano wa kudumu kati ya shauku ya mtu kwa somo fulani la utafiti na ujuzi ambao mtu anahitaji ili kusoma mada kwa njia halali ya kitaalum. Mvutano huu ni mkali zaidi kwa watafiti na wasaidizi wa utafiti wanaoishi katika eneo lao la utafiti.”

Francine Mudunga, “Epistemological rupture, detachment, and decentering: requirements when doing research ‘at home’”

NIONYESHE ZAIDI

“Itifaki za uzalishaji wa maarifa zinatuelekeza kujitenga na maeneo ya utafiti wetu kuweza kuyasoma. Lakini hii inamaanisha nini kimaadili katika maeneo masikini na zisizo salama?”

Anuarite Bashizi, “The egocentricity of field ethics: questioning otherness, decency and responsibility”

NIONYESHE ZAIDI

“Nilikuwa peke yangu na dereva ambaye alinipeleka kuona mahali ambapo kamanda wa waasi alikuwa amemuua kanali kutoka jeshi la kitaifa. Nilikuwa namfahamu Kanali mhusika kwani alikuwa mmoja wa viongozi wa jamii yangu.”

Thamani Mwaka Précieux, “Waiting for the morning birds: researcher trauma in insecure environments”

NIONYESHE ZAIDI

“Ingekuwa muhimu kuunda nafasi ya majadiliano na kubadilishana juu ya changamoto za kibinadamu za utafiti.”

François-Merlan Zaluke Banywesize, “Research, or Adventure? The lived experiences of researcher assistants”

NIONYESHE ZAIDI

“Kutoka katika hali kama hizo kunahitaji juhudi nyingi za kimkakati. Lakini pia inaweza kusababisha kuchanganyikiwa kwa muda mrefu.”

An Ansoms & Irène Bahati, “When the room is laughing: from female researcher to researcher-prostitute”

NIONYESHE ZAIDI

“Wahusika katika tabaka la kwanza wanapata ufadhili wa utafiti na kawaida huwa na udhibiti kamili juu ya mchakato wa utafiti. Wanaamua kanuni ya mwenendo na masharti ya rejeleo na kujaribu kuhakikisha kuwa kiwango cha chini cha malengo ya utafiti yatimizwa na wasaidizi wa utafiti walioajiriwa kupitia mafunzo ya muda mfupi.”

Godefroid Muzalia, “‘Businessisation of Research’ and Dominocentric Logics: Competition for Opportunities in Collaborative Research”

NIONYESHE ZAIDI

“Kujichukulia kama ndugu kwa namna fulani tuliona kuungwa mkono kulikuwa muhimu kama vile kukosolewa kwa maendeleo yetu.”

Josaphat Musamba & Christoph Vogel, “Umoja ni nguvu: towards more equitable collaborative research”

NIONYESHE ZAIDI

“Swali wanalouliza ni sawa kila wakati ‘Tutapata lini ripoti juu ya matokeo ya utafiti wako?’ Kwa ukosefu wa majibu bora, ninawaambia, (nikiwa naumia rohoni) “bado tunafikiria” Ingawa najua hakuna ripoti inayokuja. Na hii inanielemea.”

Christian Chiza Kashurha, “‘Hold on; we’re still thinking it through.’ When will we get a report on your findings?”

NIONYESHE ZAIDI

“Kukosekana kwa hatua zozote za kuwapa jamii matokeo ya utafiti wanaoshiriki, mtu anaweza kuona washiriki wakionyesha mtazamo wa kutojali na/au kukataa ambayo inaweza kuhatarisha kazi ya watafiti wa siku za usoni.”

Isaac Bubala Wilondja, “’Give Me Back My Words’: reflections on a forgotten aspect of participant follow-up”

NIONYESHE ZAIDI

“Mtafiti hawezi kulazimishwa kwenda eneo la kazi, upataji wake wa taarifa anayohitaji ili afanye utafiti mzuri daima hutegemea mapenzi mema ya washiriki wa utafiti.”

Irène Bahati, “‘Come back later.’ – ‘On what day?’ – ‘Just, come back!’”

NIONYESHE ZAIDI

“Wakati watafiti wanapogunduliwa kama wanawanyonya wahojiwa wao muda na nguvu, ni rahisi kuona jinsi gani hii inaweza kuleta shida kwa ukusanyaji wa data za kuaminika.”

Espoir Bisimwa Bulangalire, “The ‘Researcher-Glutton’: Data collection in insecure settings in the Global South”

NIONYESHE ZAIDI