Maonyesho ya mtandaoni ya Bukavu (Mijadala ya Bukavu) yanachunguza mienendo ya madaraka ya nguvu za kiutafiti baina ya watafiti kutoka nchi za kaskazini na watafiti kutoka nchi za kusini. Mijadala ya maonyesho haya ya kuona ya Blogi ya Sauti za Kimya: Mijadala ya Bukavu, ambayo inajadili jinsi maarifa yanazalishwa katika taaluma, na kuchunguza maswala ya kimaadili yanayotokea kutokana na kufanya utafiti katika maeneo yenye mizozo. Mfululizo huu ni matokeo ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Angaza, Kikundi cha Mafunzo na Usalama wa Binadamu, Kikundi cha Utafiti wa Migogoro, na Juwa; imewasilishwa na Mtandao wa Utawala katika Migogoro.

Maonyesho haya mtandaoni ni mpango unaoongozwa na programu ya Mpango wa Utafiti wa Migogoro katika Shule ya Uchumi na Sayansi ya Siasa ya London na Mtandao wa Utawala katika Migogoro. Maonyesho hayo yalipokea ufadhili kutoka Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumiya ya Madola, na Maendeleo ya Uingereza, na Chuo kikuu cha Ghent, kupitia programu ya Mpango wa Utafiti wa Migogoro. Msaada wa ziada wa tafsiri ulitolewa na Kituo cha Afrika cha Firoz Lalji  katika Shule ya Uchumi na Sayansi ya Siasa ya London.WASHIRIKA

Copyright © 2022 by bukavuseries.com and Tembo Kash. All rights reserved. This website, images, content or any portion thereof may not be reproduced or used in any manner whatsoever without the express written permission of the publisher. For more information contact: intdev.crp@lse.ac.uk

Terms of Use